ÈÓã Çááå ÇáÑÍãä ÇáÑÍíã
ÇáÍãÏ ááå ÑÈ ÇáÚÇáãíä æ ÇáÚÇÞÈÉ ááãÊÞíä æ áÇ ÚÏæÇä ÅáÇ Úáì ÇáÙÇáãíä . ÃÍãÏå ÊÚÇáì ÈãÇ åæ áå Ãåá ãä ÇáÍãÏ æ ÃÔßÑå æ ÃÓÊÛÝÑå ãä ÌãíÚ ÇáÐäæÈ æ ÃÊæÈ Åáíå ãä íåÏå Çááå ÝáÇ ãÖá áå æ ãä íÖáá ÝáÇ åÇÏí áå ÇáÞÇÆá "æ ãÇ ÃÊÇßã ÇáÑÓæá ÝÎÐæå æ ãÇ äåÇßã Úäå ÝÇäÊåæÇ" æ ÇáÞÇÆá "Þá Åä ßäÊã ÊÍÈæä Çááå ÝÇÊÈÚæäí íÍÈÈßã Çááå" æ ÃÔåÏ Ãä ãÍãÏÇ ÚÈÏå æ ÑÓæáå æ ÕÝíå ãä ÎáÞå æ Îáíáå ÈáÛ ÇáÑÓÇáÉ æ ÃÏì ÇáÃãÇäÉ æ äÕÍ ÇáÃãÉ æ ßÔÝ Çááå Èå ÇáÛãÉ Õáì Çááå Úáíå æ Úáì Âáå æ ÕÍÈå æ Óáã ÇáÞÇÆá "ÕáæÇ ßãÇ ÑÃíÊãæäí ÃÕáí".
UTANGULIZI.
KUHUSU MAKALA.
Ndugu wana ukumbi Assalamu alaikum. Kwa wingi wa heshima na taadhima, ningependa kukutangulizieni makala hii fupi kuhusu sala ya safari. Katika makala hii, nitajaribu kukunakilieni hoja za kila kundi na jawabu za wapinzani wao ili kila mtu ajue kashika nini na mwenzake kashika nini. Nimeona kwamba mas-ala muhimu ya kujadiliwa ni mas-ala matatu:
1) Nini hukumu ya kupunguza rakaa katika safari – je ni lazima kufanya hivyo au ni ruhusa tu.
2) Masafa gani ambayo mtu hulazimika kusali safari.
3) Muda gani ambao mtu anatakiwa asali safari.
Nitaanza maudhui hii kwa kuzungumzia mas-ala ya kwanza: “Nini hukumu ya kupunguza rakaa katika safari – je ni lazima kufanya hivyo au ni ruhusa tu.” Nitaigawa sehemu hii sehemu mbili. Katika sehemu ya kwanza – ambayo ndio hii tunayoanza nayo - tutazungumzia hoja za wanaosema kwamba kupunguza rakaa safarini ni wajibu. Nitatoa hoja zao, jawabu za wapinzani wao na majibu yao kwa jawabu hizo za wapinzani wao. Nitanukuu hadithi, nitatoa marejeo (references) ya kila hadithi na nitatoa uchambuzi wa sanad yake kwa ufupi. Marejeo muhimu nilioyachungulia kuhusu mas-ala haya, katika vitabu vya wanazuoni ni:
1) Sh. Al-qannubi (Ibadhi) “AL-RA-AYU AL-MU’UTABAR.”
2) Sh. Ali Yahya Muammar (Ibadhi) “AHKAMU AL-SAFAR.”
3) Al-imamu Al-salimi (Ibadhi) “SHARHU AL-JAMII AL-SAHIH” j. 1, uk. 264- 266.
4) Al-hafidh Ibn Hajar (Shafi) “FAT-HU AL-BARI” katika maelezo ya hadithi na. 350.
5) Al-imamu Al-nawawi (Shafi) “SHARHU MUSLIM” katika maelezo ya hadithi na. 1568.
6) Abu Bakr bin Mohd Al-husaini (Shafi)“KIFAYATU AL-AKHYAR” uk. 224
7) Ibn Hazm (Dhahiri) “AL-MUHALLA” j. 4, uk. 172.
8) Al-imamu Al-sayyid Abdul-husain (Shia-Ithnasharia) “MASAIL AL-FIQHIYYA) uk. 70-78.
9) Sheikh Al-mufid (Shia-Ithnasharia) “AL-MUQNA’A” uk. 91.
10) Ibn Taymiyya (Hanbali) “MAJMU’U FATAWA” j. 24, uk 8 – 13.
11) Al-shawkani (Ana madhehebu yake mwenyewe) “NAYLU AL-AWTAR” j. 3, uk. 210.
12) Al-jassas (Hanafi) “AHKAMU AL-QUR’AN” j. 2, uk. 355.
13) Al-suyuti (Hanafi) “ASBABU AL-NUZUL” uk. 88.
14) Ibn Rushdi Al-qurtubi (Maliki) “BIDAYATU AL-MUJTAHID” j. 1, uk. 310.
15) Ibn Jarir Al-tabari (Ana madhehebu yake mwenyewe) “JAMI’I AL-BAYAN” j.5, uk 283, chapa mpya.
16) Al-zamakhshari (Mu’utazili) “AL-KASHAF” j. 1, uk. 590.
17) Al-imamu Sayyid Zaid bin Ali (Zain Al-abidin Imamu wa Shia-Zaidia) “MUSNAD AL-IMAMU ZAID” uk 130 – 131.
18) “VITABU TAFAUTI VYA RIWAYA.”
Mtu anaweza kurudia vitabu hivyo ili aweze kuzikusanya hoja za kila kundi na jawabu za wapinzani wao ili kufikia “Nguvu za hoja” si “Hoja za nguvu.” Natuanze maudhui yetu kwa kutazama hukumu ya kupunguza rakaa safarini.
HUKUMU YA SALA SAFARI.
Wametafautiana wanavyoni juu ya kupunguza rakaa katika sala ya safari “Je ni rukhsa tu (ruhusa) au ni wajibu?” Wakasema baadhi yao kwamba ni rukhsa na wengine wakasema kwamba ni wajibu.
HOJA ZA WALIOSEMA KWAMBA KUPUNGUZA
NI LAZIMA: SI RUHUSA.
Waliosema kwamba kupunguza rakaa ni wajibu wanajenga hoja kwa dalili zinazofata:
MOJA NI KWAMBA MTUME (S.A.W.) katika safari zake zote alikuwa akipunguza rakaa, wala hakuna hata riwaya moja kwamba Mtume (s.a.w.) kawahi kutimiza. Na zifatazo ni baadhi ya nakala za wanavyuoni wa madhehebu tafauti, nazinukuu kutoka katika kitabu “AL-RA’AYU AL-MU’UTABAR” Cha Al-imamu Said bin Mabruk Al-qannubi:
1) Anasema Al-jassaas Al-razi Al-hanafi: “Watu hawakutafautiana kuhusu Mtume kupunguza (rakaa) katika safari zake zote katika hali ya amani na hofu, basi ikathibiti kwamba Faradhi kwa msafiri ni rakaa mbili.”
2) Na anasema Ibn Al-qudama katika “Al-mughni” “Na riwaya ni mutawatir kwamba Mtume (s.a.w.) alikuwa anapunguza (rakaa) katika safari zake, ikiwa kenda hija, umra au vitani.”
3) Anasema Ibn Taymiyyah katika “MAJMUU FATAWA” j. 24, uk. 153: “Hakunukuu kutoka kwake (Mtume s.a.w.) yeyote katika Masahaba zake kwamba Yeye (Mtume s.a.w.) kasali rakaa nne, bali Hadithi ni mutawatir kutoka kwao (Masahaba) kwamba alikuwa anasali rakaa mbili Yeye (Mtume s.a.w.) pamoja na Masahaba zake.”
4) Anasema Ibn Al-qayyim katika “ZADU AL-MIAD” alipokuwa akizungumzia matendo ya Mtume (s.a.w.) katika safari: “Na alikuwa (Mtume s.a.w.) anapunguza (sala za) rakaa nne anazisali rakaa mbili tangu anapotoka hali ya kuwa ni msafiri mpaka anaporejea madina.”
5) Anasema Al-maqbali katika “AL-MANAR” j. 1, uk. 246: “Na wala haikupokewa kinyume na hivyo (kinyume na kupunguza rakaa), nao (ndio) muongozo wa Al-khulafaa Al-rashidin (Makhalifa Waongofu) baada yake (baada ya Mtume s.a.w.).
6) Anasema mwenye kitabu “AL-MANAR” (Labda ni Sayyid Mohd Rashid Ridha au mwalimu wake Sh. Mohd Abduhu): “Na kwa ujumla ni kwamba kilichothibiti, kilichowafikiwa ni kwamba Mtume (s.a.w.) alikuwa anasali Adhuhuri na Laasiri na Isha katika safari rakaa mbili mbili.”
7) Anasema Ibn Rushd katika “AL-BIDAYA”: “Ama dalili za kimatendo…hakika yake ni yale yaliyonukuliwa kutoka kwa Mtume (s.a.w.) ya kupunguza (rakaa za) sala katika safari zake zote, na kwamba haikusihi kutoka kwake Mtume (s.a.w.) kwamba alitimiza sala katu.”
8) Anasema Sh. Al-jitali katika “AL-QAWAID” j. 1, uk. 259: “Kwamba alikuwa (Mtume s.a.w.) akipunguza katika safari zake wala haikuthibiti kutoka kwake kwamba alitimiza (rakaa za) sala kamwe.”
9) Anasema Sayyid Abdu Al-husain: “Miongoni mwao wako waliona kwamba kupunguza ndio faradhi kwa msafiri, ni lazima juu yake. Na hii ndi kauli ya (Shia) Imamiya wakiwafata Maimamu wao.” “MASAIL FIQHIYYA” uk. 73.
10) Anasimulia Zain Al-abidin kwa kusema: “…Kutoka kwa Ali (r.a.) kwamba kasema: ‘Ukisafiri Sali sala zote rakaa mbili mbili isipokuwa magharibi hakika yake ni rakaa tatu.”
11) Anasema Al-shawkani katika “AL-SAIL AL-JARRAAR”: “Haikuthibiti kutoka kwake (Mtume s.a.w.) katika safari zake zote ila kupunguza (rakaa) na hayo yamo katika Sahihi mbili (Al-bukhari na Muslim) na (vitabu) vyengevyo.” Na akasema katika “WABALU AL-GHAMAM” j. 1, uk. 248: “Na haki ni ile aliosema mtunzi kwamba kupunguza (rakaa) ni wajibu, na Hadithi zimesema wazi maana hio.” Na akasema maneno kama hayo katika “AL-DARARI AL-MUDHIYYA” j. 1, uk. 275, aliposema: “Ama wajibu wa kupunguza (ushahidi wake ni) Hadithi ya Aisha.” Mwisho wa kunuku kutoka katika kitabu cha Al-imamu Al-qannubi, pamoja na kupunguza kidogo baadhi ya sehemu kwa ajili ya kufupisha. Isipokuwa nakala namba 9 na 10, nimeziongezea mimi ili tuwe tumenukuu kutoka kwa madghehebu zote za
Kiislamu. Nakala na. 9 ni kitabu cha Shia Ithnashiria na na. 10 ni Shia-Zaidia.
1) USHAHIDI WA KWANZA:
USHAHIDI UNAOPATIKANA KATIKA MATENDO HAYO YA MTUME (S.A.W.) YA KUPUNGUZA RAKAA KATIKA SAFARI ZAKE ZOTE.
Hoja ambayo tunaipata katika matendo hayo ya Mtume (s.a.w.) ambayo kwayo tunathibitisha kwamba kupunguza rakaa katika safari ni lazima, ni kwamba Allah Subhanau Wa Taala ameitaja Sala katika Qur-an mujmalan (bila ya kuifafanua), akasema Allah: “Na simamisheni Sala na mutoe Zaka.” Kisha akamuachia Mtume Wake (s.a.w.) kazi ya kufafanua. Tazama Al-jassas “AHKAMU AL-QURAN” j. 2, uk. 358, na Al-qannubi “AL-RA-AYU AL-MU’UTABAR” uk. 16. Kwahivyo namna alivyosali Mtume ndio tafsiri au ufafanuzi wa yale ambayo yameelezwa kwa ujumla bila kufafanuliwa katika Qur-an. Na hii ni kwa msingi kwamba matendo ya Mtume (s.a.w.) ni tafsiri ya kisichofafanuliwa katika Qur-an. Na mwenwewe akabainisha zaidi kwa kusema “Salini kama munavyoniona mimi ninasali.” Kwahivyo hoja hii pekeake inatosha kubainisha kwamba kupunguza
rakaa katika safari ni lazima kwani yeye hakupata kukamilisha rakaa hata katika safari yake moja, bali katika safari zake zote kapunguza rakaa na akasema “Salini kama munavyoniona mimi ninasali.” Huu ni ushahidi kwamba kila alichokifanya katika Sala ni wajibu isipokuwa kile ambacho kuna ushahidi mwengine kwamba hicho si lazima hapo itakuwa ushahidi huo umekitoa kitu hicho katika dalili ya ujumla, kama zilivyo kanuni za usuli. Na hakuna ushahidi kwamba kupunguza ni ruhusa isipokuwa dalili ambazo ushahidi wake si sahihi kama utavyoona humu.
2) USHAHIDI WA PILI.
HADITHI YA SAYYIDA AISHA (R.A.).
Anasimulia Sayyida Aisha kwa kusema:
"ÝÑÖÊ ÇáÕáÇÉ ÑßÚÊíä ÑßÚÊíä ÝÒíÏ Ýí ÕáÇÉ ÇáÍÖÑ æ ÃÞÑÊ ÕáÇÉ ÇáÓÝÑ"
“Ilifaradhishwa Sala (mwanzo) rakaa mbili mbili, kisha ikaongezwa sala ya Hadhahr (Makazi: yaani Sala isiokuwa ya safari) na sala ya safari ikiachwa
hivyo hivyo (rakaa mbili mbili.”
TAKHRIJ YA HADITHI HIO.
Hadithi hio kaipokea Al-imamu Al-rabii “AL-JAMII AL-SAHIH” Hadithi na. 29, imekuja kwa sanad safi na fupi kabisa “Kutoka kwa Abu Ubaida kutoka kwa Jabir bin Zaid kutoka kwa Aisha.” Na akaipokea Al-imamu Ahmad bin Hanbal, “AL-MUSNAD” j. 8, uk. 457, Hadithi na. 26484, na uk. 524, Hadithi na. 26812, na hapa kuna ziada kidogo katika Hadithi hio. Na pia kaipokea katika sehemu nyengine. Na kaipokea Abu Daud “AL-SUNAN” uk. 211, Hadithi na. 1195. Na akaipokea Al-imamu Malik “AL-MUWATTAA” katika “Babu Qasri Al-salati fii Al-safar” uk. 137-138, Hadithi na. 9. Na akaipokea Al-darimi katika “AL-SUNAN” “Babu Qasri Al-salati fii Al-safar” uk. 432, Hadithi na. 5/1516. Na akaipokea Al-nasai “AL-SUNAN AL-SUGHRA” Hadithi na. 454. Na akaipokea Al-bukhari “AL-SAHIH” Hadithi na. 350. Na akaipokea Muslim “SAHIH MUSLIM”
“Kitabu Salat Al-musafirin Wa Qasruha” Hadithi na. 1/1568 na 2/1569 na 3/1570. Na Al-nasaai “AL-SUNAN AL-KUBRA” j. 1, uk. 201, Hadithi na. 313.
SANAD YA HADITHI.
Usahihi wa sanad ya Hadithi hii hauna upinzani: ni sanad sahihi bila ya khilafu. Na Hadithi hii imekuja kwa sanad tafauti. Natoa sanad moja tu kwa ajili ya kuthibitisha, nayo ni sanad ya Al-bukhari. Al-bukhari kaipokea Hadithi hii kutoka kwa:
1) Abdullah bin Yusuf naye ni Al-tanisi Abu Mohd Al-kalai Al-misri. Naye ni mpokezi thabiti, muaminifu, wala hakuna aliyemjeruhi. Tazama “TAHDHIB AL-TAHDHIB” j. 6, uk. 79, tarjama na. 174. Na Abdullah bin Yusuf kaipokea Hadithi hii kutoka kwa:
2) Al-imamu Malik bin Anas, mmoja ya Maimamu wane wakubwa wa Kisuni. Huyu hana haja ya maelezo, yeye ni Imamu maarufu, mkweli, muaminifu, mwenye uwezo wa kuhifadhi riwaya na kuzifahamu. Lakini ukipenda kujua habari zake tazama “TAHDHIB AL-TAHDHIB” j. 10, uk. 5, tarjama na. 3. Na Al-imamu Malik kaipokea Hadithi hii kutoka kwa:
3) Salih bin Kaisaan naye ni mkweli, muaminifu na madhubuti sana, wala hakuna aliyemjeruhi hata mmoja: wote wanasema: “Ni muaminifu, thabiti, mwanachuoni, n.k.” Tazama “TAHDHIB AL-TAHDHIB” j. 4. uk. 350, tarjama na. 692. Na Salih bin Kaisan kaipokea Hadithi hii kutoka kwa:
4) Ur-wa bin Zubair, mtoto wa dada ake Sayyida Aisha, naye ni bahari ya elimu, Faqihi katika Mafaqihi wa madina. Naye ni mkweli, muaminifu, mwenye kukubalika na hakujeruhiwa na mtu yeyote: wote wamemsifu kwa sifa nyingi nzuri. “TAHDHIB AL-TAHDHIB” j. 7, uk. 163, tarjama na. 352. Na Ur-wa kaipokea Hadithi hii kutoka kwa Sayyida Aisha, Mama Mtukufu, Mama wa Waumini (r.a.).
Kwa hivyo hii ni sanad sahihi kabisa, ukichanganya na sanad nyengine unapata nuru juu ya nur, kwani sanad zake nyengine pia ni kama dhahabu. Natija ni kuwa hii ni Hadithi sahihi bila ya upinzani, lakini tumetoa sanad kwa kukamilisha bahthi (utafiti).
USHAHIDI.
Ushahidi tunaoupata katika riwaya hii unaonesha kwamba kupunguza rakaa katika Sala ya safari si ruhusa bali ni lazima ni kauli ya Bibi Aisha: “ÝÑÖÊ” “Ilifaradhishwa” na kauli yake: “ÃÞÑÊ” “Ikaachwa hivyo hivyo” (yaani sala ya safari ikiachwa hivyo hivyo rakaa mbili). Kwa hivyo ni wazi kwamba kupunguza rakaa katika sala ya safari ni fardhi (lazima) si ruhusa.
UPINZANI NA MJADALA JUU YA HADITHI HII.
UPINZANI WA KWANZA.
Watetezi wa rai ya kwamba kupunguza ni ruhusa tu: si lazima, wameipinga riwaya hii kwa hoja nyingi kama inavyofata:
1) Hadithi hio inagongana na Aya inayosema:
“ÝáíÓ Úáíßã ÌäÇÍ Ãä ÊÞÕÑæÇ ãä ÇáÕáÇÉ Åä ÎÝÊã Ãä íÝÊäßã ÇáÐíä ßÝÑæÇ
“Basi hakuna ubaya juu yenu kupunguza Sala ikiwa munahofia
kwamba wale waliokufuru watakutaabisheni.”
Na hii ni kwamba wao wamelifasiri neno: “ÝáíÓ Úáíßã ÌäÇÍ Hakuna ubaya juu yenu” kuwa maana yake ni ruhusa: ukitaka kufanya hivi fanya na ukitaka kufanya hivi fanya – yote hayana ubaya. Tazama
JAWABU: Lakini wakajibiwa kwamba hakuna mgongano baina ya Aya na Hadithi kwani Aya inazungumzia kitu chengine na Hadithi inazungumzia kitu chengine – Aya inazungumzia Sala ya Khofu na Hadithi inazungumzia Sala ya safari, navyo ni vitu viwili tafauti na hukumu zake ni tafauti. Bali Sala ya Safari haikutajwa katika Qur-ani kamwe kama ilivyokuja katika Hadithi ya Ibn Umar (r.a.). Na hivi ndivyo walivyosema wanavyuoni wengi wa tafsiri kwamba Aya hii imeshuka kwa ajili ya sala ya khofu: si sala ya safari. “Miongoni mwa hao ni Ibn Jarir Al-tabari na Ibn Kathir.” Hivyo ndivyo walivyoifahamu wanavyuoni hao. Dhahiri ni kwa sababu Aya inasema: “Ikiwa mutahofia kwamba waliokufuru watakutaabisheni.” Changanya hili na Hadithi ya Ibn Umar alipoulizwa: “Ewe baba yake Abdil-rahman mbona katika Qur’an tunaona sala ya Hadhar
na sala ya khofu wala hatuoni sala ya safari.” Akasema Ibn Umar: “E mtu we! Hakika Allah ametutumia Mtume Wake na hatujui kitu, bali tunakifanya kile tulichomuona akifanya.” Kaipokea Al-rabii bin Habib Hadithi na. 187, na Ahmad, na Al-nasai, na Malik. Lakini pia ni wazi kwamba waliosema kwamba Aya hio imeshuka sala ya khofu tu ni kwa kuzingatia kwamba moja ya sababu ziliopokewa juu ya kuteremka Aya hio ni “Khofu” kama alivyonukuu Ibn Jarir katika Tafsiri yake.
Na wako baadhi ya wanavyuoni wa tafsiri wanaona kwamba Aya hii imeshuka kwa ajili ya kupunguza rakaa wakati wa safari au wakati wa safari na khofu pia. Bila shaka hawa – pamoja na kuwepo kwa neno “Khofu” katika Aya hio – pia wamezingatia kuwepo kwa maneno "ÅÐÇ ÖÑÈÊã Ýí ÇáÃÑÖ" “Idha dharabtum fii Al-ardhi” tafsiri ya neno kwa neno (literally) ni “Mukipiga katika ardhi” na maana yake ni “Mukenda katika ardhi” na kwenda katika ardhi wamekufasiri wengine kuwa ni “Kusafiri.” Tazama Al-zamakhshari “AL-KASHAF” j. 1, uk. 590. Na Abu Bakr Al-husaini “KIFAYATU AL-KHYAR” uk. 224. Na tafsiri hii inaweza kupata nguvu pia kwa riwaya ya Sayyidna Umar (r.a.) ambapo aliifahamu Aya hii kuwa ni kupunguza sala
kwa ajili ya khofu katika safari. Isipokuwa yeye alijibiwa na Mtume Mwenyewe (s.a.w.) kwamba hio ni “Sadaka Allah amekupeni, basi ipokeeni sadaka Yake.”
Hio ndio rai ya kundi la pili la wanavyuoni wa tafsiri: kwamba Aya hii imeshuka kwa ajili ya sala ya safari au sala ya safari na khofu pamoja, kwa kuzingatia kuwepo kwa maneno kuwepo kwa neno “Khofu” katika Aya hio – pia wamezingatia kuwepo kwa maneno: "ÅÐÇ ÖÑÈÊã Ýí ÇáÃÑÖ" “Idha dharabtum fii Al-ardhi” “Mukenda katika ardhi.”
Lakini tunaweza kutoa jawajibu kwa hawa kwa kusema kwamba maneno: “Kwenda katika ardhi” ni mapana zaidi kuliko maana ya kisharia ya neno safari, kwani safari katika maana yake ya kisharia ni kusafiri mahala pa masafa maalum pasipopungua maili 6 kwa mujibu wa kauli ndogo yao miongoni mwa kauli za wanavyuoni wa madhehebu za Kiislamu. Wakati maneno: “Kwenda katika ardhi” inawezekana ikiwa kwenda mahala pa maili tatu, nne au tano, nayo ni masafa ambayo mtu hasali safari. Kwahivyo “Kwenda katika ardhi” ni kitu kimoja na maana ya kisharia ya safari ni kitu chengine.
Na kwa hivyo, bila shaka – ninavyoona mimi – jawabu ya wanaosema kwamba Aya hii imeteremka kwa ajili ya sala ya khofu juu ya kuwepo kwa maneno hayo: "ÅÐÇ ÖÑÈÊã Ýí ÇáÃÑÖ" “Idha dharabtum fii Al-ardhi” “Mukenda katika ardhi” ni kuwa maneno hayo ni "æÇÞÚÉ ÇáÍÇá" “Waqi’atu Al-hal” yaani ndio hali yenyewe ilivyokuwa. Kwa lugha nyengine ni kuwa Aya imeteremka wakati
watu wako katika hali hio ya kuweko mbali na makazi yao (walikuweko katika jihad katika mji wa Usfan). Na "æÇÞÚÉ ÇáÍÇá" “Waqi’atu Al-hal” haifai kuwa ushahidi katika hali kama hii.
Mfano mzuri utaokuwekea wazi makusudio yangu, ni Aya kuhusu mtu atayeua kiwindwa cha nchi kavu naye kahirimia Haji au Umra. Allah – katika Suya 5, Aya 95 – anasema: "æ ãä ÞÊáå ãäßã ãÊÚãÏÇ" “Atayekiua (kiwindwa) miongoni mwenu kwa kukusudia” basi atalipa jazaa (fidia). Jumhur ya Umma kuanzia Masahaba hadi leo, wanasema kwamba aliyehirimia akiua kiwindwa cha nchi kavu atalipa jazaa akiwa kakusudia au hakukusudia. Wakati Aya inasema “Hali ya kuwa kakusudia.” Nini sababu yake? Anasema Al-imamu Nuru Al-din Al-salimi kwamba hii ni kwa sababu Aya hii ilimshukia mtu aliyeua kwa kukusudia ndio maana limetajwa neno ãÊÚãÏÇ Mutaammidan (hali ya kuwa ni mwenye kukusudia). Kwa hivyo hii ni "æÇÞÚÉ ÇáÍÇá" “Waqi’atu Al-hal,” na "æÇÞÚÉ ÇáÍÇá" “Waqi’atu Al-hal” haizingatiwi katika hukumu madamu lafdhi ni ya ujumla, na kwahivyo mwenye kuhirimia akiua kiwindwa hata bila ya kukusudia atalipa fidia. Halkadhalika maneno hayo: "ÅÐÇ ÖÑÈÊã Ýí ÇáÃÑÖ" “Idha dharabtum fii Al-ardhi” “Mukenda katika ardhi” ni "æÇÞÚÉ ÇáÍÇá" “Waqi’atu Al-hal.” Kwani Aya ilishuka wakati watu wako katika hali hio ya kuwa mbali na makazi yao. Huu ndio muelekeo ninaouona unafaa kuwa jawabu. Lakini huu ni uoni wangu kwa hivyo watafiti nawaufikirie kwani sikuona mwanachuoni aliotoa muelekeo huu.
Ama wanavyuoni jawabu yao ni kuwa hata tukisalim amri kwamba Aya hio imeshuka kwa ajili ya sala ya safari pia, jawabu ni kuwa ushahidi wa Aya kwamba kupunguza rakaa katika safari si lazima bali ni ruhusa ni ushahidi uliojengeka katika misingi ya Dhahir wakati ushahidi unaopatikana katika Hadithi ya Aisha ni Nassu, na Nassu na Dhahir zikigongana basi inatangulizwa Nassu kama ilivyo katika fani ya Usuli, kwa hivyo kwa mujibu wa kanuni za tafsiri, hapa inatangulizwa Hadithi.
MAELEZO KWA UFUPI KUHUSU NASSU NA DHAHIR.
Kwa sababu tunawaandikia watu wote ni vyema tueleze kwa ufupi nini Nassu na nini Dhahir ili kila mtu aweze kufahamu mas-ala haya vizuri.
Kitu muhumu na cha mwanzo kabisa kwa mtafiti au mwanachuoni au mwanafunzi wa elimu wakati wa kuielezea Aya na Hadithi, ni kutazama:
1) Daraja ya kudhiri na kujificha ya Aya au Hadithi.
2) Lengo la kibalagha la Aya au Hadithi – je hio ni amri, au ni habari au ni katazo. Kama ni amri je ni amri ya lazima au ya suna au ya ibaha (ruhusa) n.k. Kama ni katazo au habari je nini lengo la habari na katazo hilo.
Sasa daraja ya kudhiri ya andiko inaweza ikawa ni Nassu na inaweza ikaw Dhahir. Nassu ni andiko ambalo liko wazi kabisa na halina maana isipokuwa moja na ambayo iko wazi katika andiko hilo. Kwa mfano Hadithi inayosema “Sisi Mitume haturithiwi tulichokiacha ni sadaka” hili ni andiko la wazi kwamba Mitume hawarithiwi - linafamika hili katika Hadithi hio bila kuwepo kujikalifisha katika kuitafuta maana. Sasa linganisha Hadithi hio na Aya inayosema: “Na Sulaiman akamrithi Daud, akasema enyi watu sisi tumefundishwa matamshi ya ndege na tumepewa kila kitu, hakika ya hii ni fadhila ya wazi.” Aya hii “Sulaiman akamrithi Daud,” wengine wamechukua ushahidi kwamba Mitume inarithiwa, lakini ushahidi huu ni Dhahir kwani Aya inawezekana kuwa na maana hio na inawezekana kuwa alimrithi utume na elimu. Kama Aya nyengine zilivyoonesha. Kwa mfano Aya ya 32 ya Sura ya 35. Aya hio inasema “Kisha tukawarithisha Kitabu wale tulioachagua katika waja wetu.” Na bila shaka hakuna aliyerithi Kitabu cha Mungu kikawa ni mali yake, si Mitume wala si wafuasi wao. Na katika Aya za mwanzo za Surat Maryam, hapo Nabii Zakaria anaomba dua apewe mtoto atayemrithi yeye na ambaye atakirithi pia kizazi cha Ya’aqub. Tazama Aya za mwanzo za sura hiyo. Sasa je hapa itayorithiwa pia ni mali ilhali kizazi cha Ya’aqubu kimeshapita na kimesharithiwa na watoto wao. Kwa hivyo mirathi hapa ni mirathi ya utume na elimu.
Sasa ukirudi katika Aya hii: “Na Sulaiman akamrithi Daud,” utakuta kwamba Aya hii inawezekana kuwa na maana hii na inawezekana kuwa na maana hii, na hii ndio ambayo kitaalam inaitwa dhahir, kwamba maana fulani imo ndani ya andiko fulani, lakini pia andiko hilo lina maana nyengine ambayo inawezekana ikiwa ndio iliokusudiwa. Wakati – kwa upande mwengine – Hadithi: “Sisi Mitume haturithiwi tulichokiacha ni sadaka” ni andiko la wazi kwamba Mitume hairithiwi, kwani kutajwa kwa maneno “tulichokiacha ni sadaka” kunabainishwa kwamba mirathi inayozingumziwa hapa ni mirathi ya mali: si mirathi ya elimu. Sasa ilipogongana Dhahir ya Aya na Nassu ya Hadithi, kitaalamu katika kanuni za kufasiri hutangulizwa Nassu
kwani Nassu ni andiko la wazi wakati Dhahir ni andiko ambalo linawezeka kuwa na maana hii au nyengine; lilipokuja andiko la wazi ikawa muradi umebainika, na natija ni kuwa Mitume (a.s.) hairithiwi na Aya “Sulaiman akamrithi Daud” maana yake kamrithi elimu na utume sawa na dua ya Nabii Zakaria katika Aya za mwanzo za Surat Marya. Bali hata Aya yenyewe “Sulaiman akamrithi Daud” inaonyesha hivyo kwamba ni mirathi ya elimu na utume lakini maelezo juu hili yatarefusha mada na kututoa nje ya maudhui.
Sasa naturudi katika Hadithi: "ÝÑÖÊ ÇáÕáÇÉ ÑßÚÊíä ÑßÚÊíä ÝÒíÏ Ýí ÕáÇÉ ÇáÍÖÑ æ ÃÞÑÊ ÕáÇÉ ÇáÓÝÑ" “Ilifaradhishwa Sala (mwanzo) rakaa mbili mbili, kisha ikaongezwa sala ya Hadhr (isiokuwa ya safari) na sala ya safari ikaachwa hivyo hivyo (rakaa mbili mbili,” tuitazame daraja ya kudhihiri ya Haditi hio, kisha tuilinganishe na Aya “ÝáíÓ Úáíßã ÌäÇÍ Ãä ÊÞÕÑæÇ ãä ÇáÕáÇÉ Åä ÎÝÊã Ãä íÝÊäßã ÇáÐíä ßÝÑæÇ “Basi hakuna ubaya juu yenu kupunguza Sala ikiwa munahofia kwamba wale waliokufuru watakutaabisheni.” Utakuta kwamba Hadithi ni Nassu (andiko lawazi) kwamba sala mwazo wake ilifaradhishwa rakaa
mbili tu, kisha sala ya kawaida ikaongezwa na Sala ya safari ikaachwa vile vile. Hili linafahamika kwa uwazi bila mashaka katika Hadithi. Wakati sehemu ya Aya inayosema “ÝáíÓ Úáíßã ÌäÇÍ” “Hkuna ubaya juu yenu” – ambayo ndio wanayoitolea ushahidi wale wenye kusema kwamba kupunguza rakaa katika safari ni ruhusa tu – si andiko la wazi kwamba kupunguza si lazima – kule “Imefaradhishwa sala rakaa mbili” (andiko la wazi), hapa “Hakuna ubaya juu yenu kupunguza” (andiko lenye uwezekano wa namna nyingi) kwa hivyo kanuni ni kutanguliza Nassu na kuiacha Dhahir, na kwahivyo Hadithi hapa inatangulizwa kwani ni Nassu wakati maana ya Aya ni Dhahir (it bears different shades of meaning). Hii ni
jawabu moja ya wale wanye kusema kwamba kupunguza rakaa ni lazima si ruhusa.
JAWABU YA PILI.
Jawabu ya pili kuhusu Aya: “ÝáíÓ Úáíßã ÌäÇÍ Ãä ÊÞÕÑæÇ ãä ÇáÕáÇÉ Åä ÎÝÊã Ãä íÝÊäßã ÇáÐíä ßÝÑæÇ “Basi hakuna ubaya juu yenu kupunguza Sala ikiwa munahofia kwamba wale waliokufuru watakutaabisheni,” ni kuwa Aya hii ni sawa na Aya yenye kusema: "Åä ÇáÕÝÇ æ ÇáãÑæÉ ãä ÔÚÇÆÑ Çááå Ýãä ÍÌ ÇáÈíÊ Ãæ ÇÚÊãÑ ÝáÇ ÌäÇÍ Úáíå Ãä íØæÝ ÈåãÇ" “Hakika ya Safa na Mar-wa ni katika alama (za dini ya) Allah basi atayehiji au kufanya umra, HAKUNA UBAYA JUU YAKE KUZIZUNGUKA.” Aya hii inazungumzia ibada za hija na umra na kwamba
atayefanya ibada hizo “Hakuna ubaya kwake kufanya Sa’ay,” Sa’ay katika ibada hizo ni kule kuzunguka baina Safa na mar-wa. Sasa Umma umetafautiana juu ya hukumu ya mzunguko huu: je ni wajibu au suna au vipi? Jumhur wakiwemo wengi ya hao wenye kusema kwamba kupunguza rakaa katika safari ni ruhusa wanasema kwamba “Kufanya Sa’ay ni wajibu.” Suala ni kuwa vipi imekuwa wajibu kufanya Sa-ay wakati Aya inasema "ÝáÇ ÌäÇÍ Úáíå Ãä íØæÝ ÈåãÇ" HAKUNA UBAYA JUU YAKE KUZIZUNGUKA MBILI HIZO (SAFAA NA MARWA yaani kufanya Sa’ay), na vipi isiwe wajibu kupunguza rakaa katika safari wakati Aya wanayoitolea ushahidi inasema: “ÝáíÓ Úáíßã ÌäÇÍ Ãä ÊÞÕÑæÇ ãä ÇáÕáÇÉ”
“HAKUNA UBAYA JUU YENU KUPUNGUZA (RAKAA ZA) SALA” – mwote muwili limetumika neno moja na ibara moja?! Huu ni mgongano wa wazi baina ya rai mbili tofauti ziliojengeka katika Aya mbili sawa sawa! Ni wazi kwamba Aya hio: “ÝáíÓ Úáíßã ÌäÇÍ Ãä ÊÞÕÑæÇ ãä ÇáÕáÇÉ” “HAKUNA UBAYA JUU YENU KUPUNGUZA (RAKAA ZA) SALA” haina maana kwamba kupunguza ni ruhusa tu, kwani kama ilikuwa ni ruhusa tu, basi na kuzunguka Safa na Marwa pia isingelikuwa lazima wakati wale wanaosema kwamba kupunguza rakaa ni ruhusa tu, wanasema kwamba kufanya Sa’ay katika Safaa na Mar-wa ni lazima – neno moja, matumizi yale yale, lakini hukumu tafauti – ajabu ilioje!
UPINZANI WA PILI.
Kumbuka kwamba tunayoizungumzia ni Hadithi ya Sayyida Aisha (r.a.) inayosema: "ÝÑÖÊ ÇáÕáÇÉ ÑßÚÊíä ÑßÚÊíä ÝÒíÏ Ýí ÕáÇÉ ÇáÍÖÑ æ ÃÞÑÊ ÕáÇÉ ÇáÓÝÑ" “Ilifaradhishwa Sala (mwanzo) rakaa mbili mbili, kisha ikaongezwa sala ya Hadhar (isiokuwa ya safari) na sala ya safari ikaachwa hivyo hivyo (rakaa mbili mbili.” Tumeinukuu Hadithi hii kama ni ushahidi wa wale wanaosema kwamba kupunguza rakaa katika safari ni lazima: si ruhusa. Halafu tukanukuu upinzani wa kwanza uliotolewa juu ya Hadithi hii na tukatoa jawabu ya kundi la pili juu ya upinzani huo. Sasa hapa tunaendelea kwa kunukuu upinzani wa pili juu ya Hadithi hio ya Aisha.
Kwa ufupi ni kuwa upinzani wa pili ni mfupi na dhaifu kuliko uliotangulia. Ufupisho wa upinzani huo ni kuwa Hadithi hii ni Hadithi Ahadi, si Hadithi mutawatir!
JAWABU ni kuwa Hadithi Mutawatir ni sharti katika mambo ya itikadi si katika mambo ya matendo, kwa makubaliano ya wote wanaozingatiwa (wenye authority), kama ilivyo katika vitabu vya usuli na elimu ya Hadithi “ÍÏíË ÇáÃÍÇÏ íÝíÏ ÇáÚãá æ áÇ íÝíÏ ÇáÚáã” “Hadithi Ahadi anafaidisha matendo wala haifaidishi yakini (mabo ya itikadi).” Kwahivyo hoja hii haina maana kwani ni kinyume na misingi tuliokubaliana.
Anasema Al-imamu Al-qannubi: “Na kama inavyojulikana kwamba Hadithi mutawatir ni chache sana, lau ingelikuwa hapatolewi hoja katika mambo ya matendo ila kwa Hadithi Mutawatir, basi isingeliwezekana isipokuwa katika mambo kidogo, nadra.” “AL-RA’AYU AL-MU’UTABAR” uk. 20.
UPINZANI WA TATU.
Upinzani wa tatu ni kuwa Hadithi hii ya Sayyida Aisha (r.a.) inayosema: "ÝÑÖÊ ÇáÕáÇÉ ÑßÚÊíä ÑßÚÊíä ÝÒíÏ Ýí ÕáÇÉ ÇáÍÖÑ æ ÃÞÑÊ ÕáÇÉ ÇáÓÝÑ" “Ilifaradhishwa Sala (mwanzo) rakaa mbili mbili, kisha ikaongezwa sala ya Hadhar (isiokuwa ya safari) na sala ya safari ikaachwa hivyo hivyo (rakaa mbili mbili,” ni kinyume na matendo yake Sayyida Aisha (r.a.).
JAWABU ni kuwa:
a) Kugongana kwa matendo ya Sahaba na rai yake hakuifanyi riwaya iwe dhaifu ikiwa riwaya hio imethibiti kwa sanad sahihi, kwani hoja ni marfuu (Hadithi ilionasibishwa na Mtume): wala hoja si mawquf (Hadithi ilionasibishwa na sahaba). Na kwenda kinyume na riwaya huenda ikawa sababu yake ni kusahau, kuiletea tafsiri riwaya hio, au sababu nyengine.
b) Pili ni kuwa Sayyida Aisha kasali hivyo si kwamba hakuna riwaya hio bali aliiletea tafsiri riwaya hio, kama alivyosema mtoto wa ndugu yake Ur-wat bin Zubair. Amepokea Al-imamu Muslim kutoka kwa Al-zuhri kasema nilimwambia Ur-wa kwanini Aisha anasali kamili (hapunguzi rakaa) akamwambia: “Hakika yake ameleta tafsiri kama alivyofanya Uthman.”
c) Tatu ni kuwa riwaya yake ni muthbit (inathibitisha sharia) wakati rai yake ni naafi (inakataa) na muthbit ikigongana na nafi basi muthbit ndio inayotangulizwa, na hivi ndivyo wanavyosema Jumhuri ya wanavyuoni wa usuli.
d) Ikigongana kauli na matendo na zikawa daraja moja basi inatangulizwa ya mwanzo. Sasa hapa kuna mgongano wa kauli na matendo, na kauli daraja yake ni kubwa zaidi kwani ni Hadithi marfuu (kutoka kwa Mtume s.a.w.), kwahivyo ni lazima itangulizwe.
e) Matendo yake yanagongana na matendo ya Masahaba wengine, na matendo ya Jumhur ya Masahaba ni bora zaidi kuliko matendo ya Sahaba mmoja.
f) Riwaya yake inapata nguvu kwa dalili nyengine wakati matendo yake hayana ushahidi wowote.
Na ni vyema kusema kwamba wanavyuoni wengine wa Kisuni wanaona kwamba mas-ala ya Aisha kupunguza sala hayakuthibiti kamwe. Anasema Ibn Taymiyya: “Hadithi hii (yaani hadithi ya kwamba Aisha kasali kamili katika safari) ni uwongo, haiwi kwa Aisha kwamba asali kinyume na Mtume (s.a.w.) na Masahaba wengine naye anawaona wanapunguza (rakaa) kisha yeye atimize bila sababu. Vipi basi (afanye hivyo) naye ndiye aliyesema: “Ilifaradhishwa Sala (mwanzo) rakaa mbili mbili, kisha ikaongezwa sala ya Hadhar (isiokuwa ya safari) na sala ya safari ikaachwa hivyo hivyo (rakaa mbili mbili.” Kayanukuu maneno haya Al-qannubi katika “AL-RA-AYU AL-MU’UTABAR” uk. 61. Na mfano wake katika “AHKAMU AL-SAFAR” cha Sh. Ali Yahya Muammar, uk. 41. Na anasema Ibn Hazm katika “AL-MUHALLA” j. 4, uk. 176 kuhusu riwaya kwamba Aisha kasali kamili
katika safari: “Ama riwaya mbili hazina kheri.” Hayo ndio maneno ya Ibn Hazm, kama unavyojua Ibn Hazm hana lugha nyepesi nyepesi. Na anasema Al-shawkani “Ama hadithi ya Aisha…kwamba yeye katimiza (rakaa za) sala katika safari, yatakuja (maelezo) kwamba (riwaya hio) haikusihi.” “NAYLU AL-AWTAR” j. 3, uk. 211.
UPINZANI WA NNE.
Upinzani wa nne ni kuwa Hadithi hii ya Aisha: "ÝÑÖÊ ÇáÕáÇÉ ÑßÚÊíä ÑßÚÊíä ÝÒíÏ Ýí ÕáÇÉ ÇáÍÖÑ æ ÃÞÑÊ ÕáÇÉ ÇáÓÝÑ" “Ilifaradhishwa Sala (mwanzo) rakaa mbili mbili, kisha ikaongezwa sala ya Hadhar (isiokuwa ya safari) na sala ya safari ikaachwa hivyo hivyo (rakaa mbili mbili,” inagongana na Hadithi ya Ibn Abbas inayosema: “Hakika ya Sala imefaradhishwa rakaa nne katika Hadhar (sala ya kawaida) na rakaa mbili katika safari.”
JAWABU ni kuwa:
a) Hakuna mgongano baina ya riwaya mbili hizo kwani riwaya ya Ibn Abbas haina ndani yake ubainifu uliomo katika riwaya ya Aisha. Hadithi ya Aisha inabainisha kwamba Sala mwanzoni ilikuwa rakaa mbili kisha sala ya kawaida ikazidishwa na sala ya safari ikaachwa kama ilivyo. Wakati Hadithi ya Ibn Abbas inasema: “Sala imefaradhishwa rakaa mbili safarini na rakaa nne katika Hadhar.” Kwa hivyo hapa hakuna kugongana kwani Aisha anazungumzia kitu chengine na Ibn Abbas anazungumzia kitu chengine: Aisha anazungumzia hali ilivyokuwa mwanzo na ilivyokuwa hatimae wakati Ibn Abbas Hadithi yake haikutoa ufafanuzi hio, dhahiri ni kuwa yeye anazungumzia hali ya sala ilivyo sasa au kwa maneno mengine hali yake ya
mwisho tu.
b) Lakini hata tukisema kwamba kuna mgongano baina ya Hadithi ya Aisha na Ibn Abbaas, JAWABU ni kuwa Hadithi ya Ibn Abaas ni Mujmal (haina ufafanuzi) na Hadithi ya Aisha ni Mubayyan (ina ufafanuzi) na Mujmal ikigongana Mubayyan, basi inayotangulizwa ni Mubayyan kama ilivyo katika kanuni za Usuli-lfiq-hi.
UPINZANI WA TANO.
Upinzani wa tano wa Hadithi hio ya Aisha: "ÝÑÖÊ ÇáÕáÇÉ ÑßÚÊíä ÑßÚÊíä ÝÒíÏ Ýí ÕáÇÉ ÇáÍÖÑ æ ÃÞÑÊ ÕáÇÉ ÇáÓÝÑ" “Ilifaradhishwa Sala (mwanzo) rakaa mbili mbili, kisha ikaongezwa sala ya Hadhar (isiokuwa ya safari) na sala ya safari ikaachwa hivyo hivyo (rakaa mbili mbili,” ni kuwa Hadithi hii inagongana, kwani kaipokea Ibn Ajlan kutoka kwa Salih bin Kaisan kutoka kwa Ur-wa kutoka kwa Aisha akisema: “Kafaradhisha Mtume (s.a.w.) Sala rakaa mbili mbili” na akasema Al-awzai kutoka kwa Ur-wa kutoka kwa Aisha: “Allah kafaradhisha Sala rakaa mbili mbili.”
JAWABU ni kuwa hakuna mgongano kwa sababu maandiko huwa hayaesabiwi kwamba yanagongana ila katika hali mbili:
1) Iwe haiwezekani kulipa uzito andiko moja dhidi ya jengine, na hapa inawezekana kwani Al-awzai si madhubuti: Al-imamu Ahmad bin Hanbal kamdhaifisha, kwahivyo riwaya yake haiisabiwi kwamba inagongana na riwaya ya pili, kwani riwaya haziambiwi kwamba zinagongana mpaka sanad zake siwe sawa katika usahihi.
2) Iwe haiwezekani kuyajumuisha maandiko hayo. Na hapa – tukijaalia kuwa riwaya zote ni sahihi basi - inawezekana kuzijumuisha kwani maana ya “Mtume kafaradhisha” ni sawa na “Allah kafaradhisha” kwani Allah ndio Mwenye kutoa sharia na Mtume ni mfikishaji. Na kwa maana hii ndio Qur-an inasema “Atayemtii Mtume basi kamtii Allah.” Bali riwaya hii imekuja kwa lafdhi nyengine nayo ndio hio tulioinukuu mwanzo, yaani lafdhi inayosema “Ilifarashwa Sala.”
UPINZANI WA SITA.
Upinzani wa sita ni kuwa Hadithi hii: "ÝÑÖÊ ÇáÕáÇÉ ÑßÚÊíä ÑßÚÊíä ÝÒíÏ Ýí ÕáÇÉ ÇáÍÖÑ æ ÃÞÑÊ ÕáÇÉ ÇáÓÝÑ" “Ilifaradhishwa Sala (mwanzo) rakaa mbili mbili, kisha ikaongezwa sala ya Hadhar (isiokuwa ya safari) na sala ya safari ikaachwa hivyo hivyo (rakaa mbili mbili,” ni kauli ya Aisha: si kauli ya Mtume (s.a.w.).
JAWABU ni kuwa Hadithi ya Sahaba huisabiwa kuwa ni mawqufu (yenye kutoka kwa sahaba) ikiwa ni kitu ambacho kinawezekana kuwa rai ya sahaba: ama ikiwa kitu ambacho hakiwezekani kuwa rai ya sahaba, basi Hadithi anayoitamka sahaba bila kumtaja Mtume (s.a.w.) hukumu yake huwa ni Hadithi ya Mtume (s.a.w.) hata ikiwa hakusema Sahaba huyo kwamba Mtume (s.a.w.) kanena au katenda. Hivi ndivyo misingi ya Hadithi, tafsiri na fiq-hi inavyosaema. Kwahivyo Hadithi hii hukumu yake ni Marfuu (kutoka kwa Mtume s.a.w.) kwani mas-ala haya hayatoi nafasi ya kutoa rai – hakuna mtu anayeweza kusema kwamba rai yake ni kuwa sala ilifaradhishwa rakaa mbili halafu ikizidishwa: haya ni mas-la yanayotegemea Shahada (Kushuhudia) au habari sahihi kutoka kwa waaminifu. Kwa hivyo hii si Hadithi ya Aisha bali ni Hadithi ya Mtume (s.a.w.),
au kwa lugha ya kitaalamu hii si Hadithi mawqufu bali ni Hadithi Marfuu.
UPINZANI WA SABA.
Upinzani wa Saba uliotolewa juu ya Hadithi hii: "ÝÑÖÊ ÇáÕáÇÉ ÑßÚÊíä ÑßÚÊíä ÝÒíÏ Ýí ÕáÇÉ ÇáÍÖÑ æ ÃÞÑÊ ÕáÇÉ ÇáÓÝÑ" “Ilifaradhishwa Sala (mwanzo) rakaa mbili mbili, kisha ikaongezwa sala ya Hadhar (isiokuwa ya safari) na sala ya safari ikaachwa hivyo hivyo (rakaa mbili mbili,” ni kawa Aisha hakuzidiriki zama za kufaradhishwa Sala!
JAWABU ni kuwa huu ndio upinzani dhaifu wao, kwani hata kama yeye hakudiriki zama za kufaradhishwa sala, hii maana yake ni kuwa Hadithi yake hii ni Mursal Al-sahabi na Mursal Al-sahabi ni hoja katika hoja za kisharia. Lakini tumetanguliza kusema kwamba haya si mas-ala ya rai, haiwezekani kuwa ni rai ya Sayyida Aisha (r.a.).
Jawabu hio ni sahihi ikiwa tutakubali kwamba Sayyida Aisha hakuidiriki zama za kufaradhishwa sala, vyenginevyo tunasema kwamba Aisha (r.a.) kadiriki zama za kufaradhishwa sala, kwani sala imefaradhishwa naye ni mdogo yupo tayari katika nyumba ya baba yake Abu Bakr (r.a.), na riwaya iliopokelewa na mtoto mwenye fahamu inakubalika ikiwa ataisimulia baada ya kubaleghe kama ilivyo katika elimu ya Hadithi, nayo ndio madhehebu ya Jumhuri ya wanavyuoni wa usuli na Hadithi. Na riwaya kama hizo ziliopokewa na Masahaba walipokuwa wadogo wakazisimulia baada ya kubalegh ziko nyingi, kama riwaya za Ibn Abbas, Ibn Umar na wengine wengi. Kwa hali yoyote ile haya yote ni majibu ya kujaalia tu, vyengivyo Hadithi hio ya Aisha sigha (form) yake ni Mursal na Mursal ya Sahaba ni hoja: na maana yake ni Marfuu
(kutoka kwa Mtume s.a.w.) na Hadithi ya Sahaba ikiwa maana yake ni Marfuu, basi hukumu yake huwa ni Marfuu (inatoka kwa Mtume s.a.w.).
HATIMA NA MUKHTASARI.
1) Maudhui yetu katika sehemu hii ya makala ni kuhusu kupunguza rakaa katika safari – je ni lazima au ni ruhusa tu?
2) Baadhi ya Waislamu wanaona kwamba hio ni ruhusa tu na baadhi wanaona kwamba hio ni lazima.
3) Wanaona kwamba hio ni lazima wanajenga hoja kwa riwaya ya Sayyida Aisha inayosema: "ÝÑÖÊ ÇáÕáÇÉ ÑßÚÊíä ÑßÚÊíä ÝÒíÏ Ýí ÕáÇÉ ÇáÍÖÑ æ ÃÞÑÊ ÕáÇÉ ÇáÓÝÑ" “Ilifaradhishwa Sala (mwanzo) rakaa mbili mbili, kisha ikaongezwa sala ya Hadhar (isiokuwa ya safari) na sala ya safari ikaachwa hivyo hivyo (rakaa mbili mbili,” pamoja na matendo ya Mtume (s.a.w.) kwamba yeye hakuwahi hata siku moja kusali kamili katika safari, na hili halina khilafu katika Umma.
4) Wanaoona kwamba kupunguza ni ruhusa tu: si lazima, wamejibu kwa hoja ambazo tumezinukuu, na wapinzani wao wamejibu kwa hoja ambazo tumezinukuu pia.
5) Upinzani walioutoa wale wanaona kuwa hio ni ruhusa, si madhubuti kwani kila hoja yao moja ni kinyume na kanuni za kiusuli na kanuni za elimu ya Hadithi ambazo ndizo tunazojiongozea katika kuifasiri Qur-an na Suna za Mtume (s.a.w.), na aliyesoma fani hizo anaona hivyo kwa uwazi katika majibizano haya au mjadala huu.
6) Kwa hivyo tunaishia kwa kusema kwamba Hadithi hii ya Aisha imethibitisha ulazima wa kupunguza rakaa katika safari, na hakuna hoja madhubuti ya kuipinga, kwa hivyo tunasema kwamba Hadithi: “Ilifaradhishwa Sala (mwanzo) rakaa mbili mbili, kisha ikaongezwa sala ya Hadhar (isiokuwa ya safari) na sala ya safari ikaachwa hivyo hivyo (rakaa mbili mbili,” ukichanganya na hoja ya kwanza kwamba Mtume (s.a.w.) hajawahi kukamilisha rakaa katika sala ya safari tunapata kwamba kupunguza rakaa ni wajibu kwa mujibu wa suna ya kauli na suna ya vitendo.
USHAHIDI WA PILI.
Ushahidi wa pili ambao unaonesha kwamba kupunguza rakaa katika Sala ya safari ni lazima, ni Hadithi ya Ibn Abbasa (r.a.) inayosema:
"ÝÑÖ Çááå ÇáÕáÇÉ Ýí ÇáÍÖÑ ÃÑÈÚÇ æ Ýí ÇáÓÝÑ ÑßÚÊíä"
“Allah kaifaradhisha Sala ya Hadhar (ya kawaida) rakaa nne, na katika safari rakaa mbili.”
TAKHRIJ.
Kaipokea Al-imamu Muslim katika “AL-SAHIH” Hadithi na. 5/1573, na 6/1573 katika “Kitabu Salat Al-musafirin Wa Qasruha.” Na akaipokea Ibn Maja “AL-SUNAN” uk. 180, Hadithi na. 1068. Na akaipokea Al-imamu Ahmad “AL-MUSNAD” j. 1, uk. 631, Hadithi na. 2124 na uk. 644, Hadithi na. 2177, na uk. 669, Hadithi na. 2293 na uk 888, Hadithi na. 3332. Na akaipokea Al-nasaai katika “AL-SUNAN AL-KUBRA” j. 1, uk. 201, Hadithi na. 314, na uk. 278, Hadithi na. 514, na j. 2, uk. Hadithi na. 1912 na uk. 360, Hadithi na. 1913. Na akaipokea pia Ibn Hazm katika “AL-MUHALLA” j. 4, uk. 177, na j. 5, uk. 31. Hao ndio wapokezi niliobahatika kuvichungulia vitabu vyao. Na hapa kuna wapokezi wengine ambao sikuwahi kuvirejea vitabu vyao, kawanukuu Al-imamu Al-qannubi katika “AL-RA-AYU AL-MU’UTABAR” uk. 26, na pia
kawanukuu mtiaji maelezo wa “SHARH AL-NAWAWI ALAA SAHIHI MUSLIM” j. 4, uk. 7, maelezo na. 687. Nao ni: “Abu Ya’ala, Al-bayhaqi, Al-imamu Al-shafi katika “AL-SUNAN AL-MANTHURA,” Al-tabrani, Ibn Jarir Al-tabari, Al-tahawi katika “SHARHU AL-MAANI”, Ibn Khuzaima, Ibn Hibban, Abu Awana, na wengineo.”
SANAD YA HADITHI.
Katika sanad zote nilizozipitia sikuona isipokuwa “ ãÌÇåÏ Úä ÇÈä ÚÈÇÓMujahid An Ibn Abbas yaani Mujahid kutoka kwa Ibn Abbas.” Hii kitaalam inaitwa Hadithu Mu’an’an yaani hadithi ambayo msimulizi wake anatumia lafdhi Úä An (kutoka). Hadithi kama hii inakuwa sahihi ikiwa mpokezi si mwenye kughushi. Ama Mujahid ni Imamu mkubwa sana, mwingi wa elimu lakini hakusalimika na jaraha hili. Al-tirmidhi aripoti kwamba “MUJAHID ni maarufu kwa kughushi.” Tazama “TAHDHIB AL-TAHDHIB” juzuu ya 10 ukurasa wa 38-40, tarjama ya 68. Kwahivyo dhati ya sanad hii si
sahihi, lakini hadithi yenyewe ni sahihi, kwani Hadithi ya mwenye kughushi (ikiwa si Tadlis Al-ttas-wiya) ikipokewa kwa njia nyengine dhaifu kidogo inapanda daraja na kufika Hasan lighairihi. Hadithi Hasan ni Hadithi iliochini ya hadithi sahihi kidaraja lakini zote zinafaa. Sasa hadithi hii ya Mujahid imekuja kwa njia sahihi nayo ni njia ya Sayyida Aisha tuliotangulia kuinukuu. Kwa hivyo natija ni kuwa hii ni hadithi sahihi, na kwa hivyo ndio maana wanavyuoni wakubwa wa fani ya hadithi wameitolea hoja.
USHAHIDI.
Ushahidi ambao tunaupata katika Hadithi hii wenye kuonesha kwamba kupunguza rakaa ni wajibu, ni sawa na ushahidi tunaoupata katika Hadithi ya Sayyida Aisha. Hadithi zote mbili zinasema kwamba “Sala ya kawaida imefaradhishwa rakaa nne na Sala ya safari imefaradhishwa rakaa mbili.” Kwa hivyo fardhi au kilicho wajibu katika safari ni rakaa mbili, yaani kwa Sala zile zenye rakaa nne. Hatuna haja ya kuijadili Hadithi hii kwani maana yake ni sawa na Hadithi iliotangulia.
USHAHIDI WA TATU.
Ushahidi wa tatu ni Hadithi ya Umar inayosema:
"ÕáÇÉ ÇáÝØÑ ÑßÚÊÇä æ ÕáÇÉ ÇáÃÖÍì ÑßÚÊÇä æ ÕáÇÉ ÇáÌãÚÉ ÑßÚÊÇä æ ÕáÇÉ ÇáÓÝÑ ÑßÚÊÇä
ÊãÇã ÛíÑ ÞÕÑ Úáì áÓÇä ãÍãÏ Õáì Çááå Úáíå æ Óáã"
“Sala ya Idi-l-fitri ni rakaa mbili, na sala ya Idi-l-adh-ha ni raka mbili na Sala ya Ijumaa ni rakaa mbili na Sala ya safari ni rakaa mbili kamili, haikupungua kwa maneno ya Muhammad (s.a.w.).”
TAKHRIJ
Hadithi hio kaisimulia Al-imamu Ahmad bin Hanbal katika “AL-MUSNAD” j. 1, uk. 154, hadithi na. 257. Na akaipokea Ibn Maja “AL-SUNAN” uk. 179, hadithi na. 1063 na 1064. Na akaipokea Abu Daud Al-tayalisi “AL-MUSNAD” uk. 20, hadithi na. 136. Na akaipokea Abdu bin Humaid “AL-MUNTAKHAB MIN MUSNAD ABDI BIN HUMAID” uk. 40, hadithi na. 29. Na Abdu Al-razaaq Al-san’ani katika “AL-MUSANNAF” j. 2, uk. 342, hadithi na. 3289, na mfano wake ni hadithi na 4290, na 4292. Na Al-bazzar katika “AL-BAHRU AL-ZAKHAAR” j. 1, uk. 465, hadithi na. 331. Na Abu Ya’ala “AL-MUSNAD” j. 1, uk. 88, hadithi na. 241. Na wengineo ambao kawataja Al-imamu Al-qannubi sikuvirejea vitabu vyao kuhakikisha ni: “Al-nasaai, Abu Nuaim na Al-tahhawi.” Na wengine kawataja mtiaji maelezo wa “AL-MUSNAD” cha Al-imamu Ahmad ambao pia sikuvirejea vitabu vyao ni: “Ibn Khuzaima na Ibn Abi Shaiba.”
SANAD YA HADITHI.
Hadithi hii imekuja kwa sanad nyingi, na hakuna sanad mbaya sana, bali aghlabu ya sanad zake ni dhaifu kidogo ambazo zinapanda daraja kwa sababu ya kupeyana nguvu zenyewe kwa zenyewe. Lakini mimi nanukuu sanad ilio sahihi tu, nayo ni sanad ya Ibn Maja.
Ibn Maja kaipokea hadithi hii kutoka kwa:
1) Mohd bin Abdi-llahi bin Numair, naye ni mkweli, muaminifu, madhubuti sana, mwingi wa elimu na ucha Mungu, wala hakuna aliyemjeruhi: wote wamemsifu kwa sifa nzuri sana. Tazama: “TAHDHIB AL-TAHDHIB” j. 9, uk. 251, tarjama ya 465. Na Moh’d bin Abdillah bin Numair kaipokea hadithi hii kutoka kwa:
2) Mohd bin Bishr, naye ni mkweli muaminifu wala hakuna aliyemjeruhi isipokuwa hadithi zake alizozipokea kutoka kwa Mujahid tu ndio kuna aliyedai kwamba ni Mursal. “TAHDHIB AL-TAHDHIB” j. 9, uk 64, tarjama na. 90. Na Mohd Bin Bishr kaipokea hadithi hii kutoka kwa:
.
3) Yazid bin Abi Ziyad bin Abi Ja’ad, naye ni muaminifu, wala hakuna aliyemjeruhi. “TAHDHIB AL-TAHDHIB” j. 11, uk. 286, tarjama na. 528. Na Yazid kaipokea hadithi hii kutoka kwa:
4) Zubaid bin Al-harith, naye ni muaminifu, thabiti wala hakuna aliyemjeruhi. “TAHDHIB AL-TAHDHIB,” j. 3, uk. 268, tarjama ya. 578. Na Zubaid kaipokea hadithi hii kutoka kwa:
5) Abdul-rahman bin Abi Laila, naye ni imara, thabiti, muaminifu, Imamu, wala hakuna aliyemjeruhi. “TAHDHIB AL-TAHDHIB,” j. 6, uk. 234, tarjama ya 518. Na Abdul-rahman kaisikia hadithi hii kutoka kwa:
6) Ka’ab bin Ujrah, huyu ni Sahaba mtakatifu; hana haja ya maelezo. Naye kaisimulia hadithi hii kutoka kwa:
7) Umar bin Al-khattaab æ ãÇ ÃÏÑÇß ãÇ ÚãÑWa maa adraka maa Umar (na nini kinakujuilisha wewe: Umar ni nani)? Iulize historia ya haki na uadilifu, itakujibu Umar ni nani. Allah amuwiye radhi na kumuingiza katika Firdausi ya juu.
Hii ndio sanad ya hadithi hii, nayo kama unavyoona ni dhahabu kutoka kwa dhahabu. Isipokuwa kuna kitu kimoja ningependa kukitolea TANBIHI. Nacho ni kuwa kuna tafauti ya wanavyuoni: je Abdul-rahman bin Abi Laila (mpokezi na. 5) kasikia hadithi kutoka Sayyina Umar? Wengine wanasema hakusikia bali baina yao kuna Ka’ab bin Ujra kama ilivyo sanad hii, na pia yupo baina yao Al-baraau bin Aazib.
Na wengine wanasema kwamba bali kasikia hadithi kutoka kwa Umar. Na kauli hii ndio alioipasisha Sh. Al-qannubi katika wanavyuni wakubwa wa hadithi wa sasa. Na mimi – si mwanachuni lakini – napendezewa na kauli hii kwa sababu Abdul-rahman ni muaminifu kwa makubaliano ya wote naye kasema kwa uwazi “Nimemsikia Umar.” Tazama “AL-MUSNAD” cha Al-imamu Ahmad bin Hanbal, j. 1, uk. 155, katika maelezo yanayofata chini ya hadithi na. 257. Sasa kama mwenye anasema “Nimemsikia” naye ni mkweli muaminifu kwa ushahidi wa wanavyuoni wa hadithi hakuna maana ya kusema kwamba hakusikia hadithi kutoka kwa “Umar.” Kwahivyo kauli ya waliosema kwamba kasikia hadithi kutoka kwa Sayyidna Umar ndio kauli sahihi. Kwahivyo riwaya nyengine ambazo hakumtaja Ka’ab bin Ujra bali kasema “Kutoka kwa Umar” ni riwaya sahihi pia. Na kwa maana hii itakuwa hadithi hii ni katika "ÇáãÒíÏ Ýí ãÊÕá ÇáÃÓÇäíÏ" Al-mazid fii muttasil Al-asaniid yaani hadithi ambayo sanad yake imeungana kisha akaongezeka mpokezi mwengine wa ziada, nayo ni kasoro ambayo haivunji usahihi wa hadithi "ÚáÉ ÛíÑ ÞÇÏÍÉ Ýí ÕÍÉ ÇáÍÏíË".
USHAHIDI.
Nadhani Hadithi iko wazi kwamba sala ya safari ni rakaa mbili. Ni wazi kwamba kupunguza si ruhusa, bali ni wajibu.
USHAHIDI WA NNE.
Ushahidi wa nne ni Hadithi ya Ya’ala bin Umayya inayosema:
"ÞáÊ áÚãÑ Èä ÇáÎØÇÈ ÑÖí Çááå Úäå (ÝáíÓ Úáíßã ÌäÇÍ Ãä ÊÞÕÑæÇ ãä ÇáÕáÇÉ Åä ÎÝÊã) æ ÞÏ Ããä ÇáäÇÓ , ÝÞÇá: ÚÌÈÊ ããÇ ÚÌÈÊ ãäå ÝÓÃáÊ ÑÓæá Çááå Õáì Çááå Úáíå æ Óáã ÝÞÇá: "ÕÏÞÉ ÊÕÏÞ Çááå ÈåÇ Úáíßã ÝÃÞÈáæÇ ÕÏÞÊå"
“Nilimwambia Umar bin Al-khattaab (r.a.) (Allah anasema) Hakuna ubaya juu yenu kupunguza (rakaa za) sala mukihofia.” Na sasa watu wako katika amani (basi vipi wapunguze rakaa). Akasema (Umar r.a.): “Nimestaajabu kama ulivyostaajabu nikamuuliza Mtume (s.a.w.) akasema: (Hio ni) Sadaka
Allah amekupeni basi ikubalini sadaka yake.”
TAKHRIJ
Hadithi hii kaipokea Al-imamu Muslim “SAHIHU MUSLIM” hadithi na. 4/1571. Na Ibn Maja “AL-SUNAN” uk. 180, hadithi na. 1065. Na Al-tirmidhi “AL-SUNAN” uk. 806, hadithi na. 3034. Al-darmi “AL-SUNAN” uk. 431, hadithi na. 1512. Al-imamu Ahmad “AL-MUSNAD” j. 1, uk. 128 hadithi na. 174 na uk. 151, hadithi na. 244 na 245. Abu Ya’ala “AL-MUSNAD” uk. 181, hadithi na. 181. Al-bayhaqi “AL-SUNAN AL-SUGHRA” j.1, uk. 240, hadithi na. 497. Na wengineo.
SANAD YA HADITHI.
Hadithi hii imekuja kwa sanad tafauti. Na kwa upekuzi wa haraka haraka naona sanad bora ni sanad ya Al-tirmidhi na Al-imamu Ahmad bin Hanbal. Nanukuu sanad ya Al-imamu Ahmad. Al-imamu Ahmad kaipokea hadithi hii kutoka kwa:
1) Yahya naye ni Yahya bi Said Al-qattaan, naye ni Imamu mkubwa mwingi wa elimu, mkweli, muaminifu mwenye hifadhi kali. Anasema Al-imamu Ahmad bin Hanbal “Walahi hatukumkuta mtu mfano wake.” Na anasema tena “Alikuwa ndio kipeo cha uthabiti (uimara) kati Basra.” Na kwa ufupi sifa zake ni refu wala hakuna aliyemjeruhi. “TAHDHIB AL-TAHDHIB” j. 11, uk. 190, tarjama na. 359.
2) Ibn Juraij. Jina lake ni Abdul Malik bin Abdul Aziz bin Juraij. Huyu ni Imamu mkubwa, mwingi wa elimu na riwaya lakini pia ni mwingi wa kughushi. Lakini hadithi ya Mudallis (anayeghushi) huwa dhaifu ikiwa atatumia lafdhi ambayo haimaanishi kwamba yeye kaisikia hadithi hio kwa mpokezi aliye juu yake. Kwa mfano akisema: "Úä ÝáÇä Ãæ Ãä ÝáÇäÇ ÞÇá" “An Fulani Au Anna Fulanan Qala” “Kutoka kwa fulani” au akisema: “Kwamba fulani kasema,” au lafdhi yoyote ile ambayo haioneshi kwamba yeye kaisikia hadithi hio kutoka kwa mpokezi aliye kabla yake. Ama katika hadithi hii, Ibn
Juraij kasema kwa uwazi “Kanisimulia Abdul-rahman” kama ilivyo riwaya ya Al-imamu Ahmad bin Hanbal na Abu Ya’ala. Na akasema: “Nimemsikia Abdul-rahman” kama ilivyo riwaya ya Al-tirmidhi. Tazama habari Ibn Jurai katika “TAHDHIB AL-TAHDHIB” j. 6, uk. 357, tarjama na. 758.
3) Abdul-rahman bin Abdillah bin Abi Ammar, naye ni muaminifu wala hakuna aliyemjeruhi. “TAHDHIB AL-TAHDHIB” j. 6, uk. 194, tarjama na. 433.
4) Abdullah bin Babaihi na wengine wanamwita Abdullah bin Babi na wengine wanamwita Abdullah bin Babahu, naye ni muaminifu, kama alivyosema Al-nasai. Tazama “TAHDHIB AL-TAHDHIB” j. 5, uk. 133, tarjama ya 261.
5) Ya’ala bin Umayya. Huyu ni Sahaba (r.a.).
6) Umar bin Al-khattab (r.a.).
Kwa hivyo hii ni sanad sahihi: haina tatizo lolote.
USHAHIDI.
Kinachoonesha ulazima wa kupunguza rakaa katika safari katika riwaya hii ni maneno ya Mtume (s.a.w.) aliposema “Ikubalini sadaka Yake.” Na hii ni kwa kuzingatia kwamba neno: “Ikubalini” ni Amri na Amri “íÞÊÖí ÇáæÌæÈ ãÇ áã ÊÕÑÝå ÞÑíäÉ” Inamaanisha wajibu madamu hakuna Qarina (context) ilioigeuza (amri hio kuotoka katika huo wajibu). Al-jassas “AHKAMU AL-QURAN” j. 2, uk. 358, na Al-qannubi “AL-RA-AYU AL-MU’UTABAR” uk. 27. Hii ni kanuni (law) ya kiusuli (fandumentals of Islamic Jurisprudence), na maana yake ni kuwa popote pale ambapo Allah au Mtume (s.a.w.) wanatoa amri basi amri hio ni wahibu kutekelezwa isipokuwa pale ambapo kuna kilichoonesha kwamba amri hio si amri ya lazima. Ama neno “Sadaka” halioneshi kwamba kupunguza si
lazima kwa sababu mas-ala hapa si kuwa sisi ndio tutoe sadaqa, “Laa” bali tunachoamrishwa na Mtume (s.a.w.) ni kuwa sisi tuipokee sadaka ya Allah. Zingatia wewe lau upo mbele ya Mtume (s.a.w.) akaja mtu akakupa sadaka, Mtume (s.a.w.) akakwambia: “Ipokee” je inajuzu kutokuipokea? Aliyetoa sadaka kwa asili hakulazimika kufanya hivyo, lakini mpokeaji kalazimika kupokea kwa sababu ya Amri ya Mtume (s.a.w.). Kwa hivyo hii ni Amri ya Mtume na AMRI: “íÞÊÖí ÇáæÌæÈ ãÇ áã ÊÕÑÝå ÞÑíäÉ” Inamaanisha wajibu madamu hakuna Qarina (context) ilioigeuza (amri hio kuotoka katika huo wajibu. Kwa hivyo kupunguza ni wajibu katika safari kwani Mtume (s.a.w.) katuamrisha tukupokee. Anasema Allah “Na atachokupeni Mtume kichukuweni, na atachokukatazeni basi katazikeni nacho.” Sura 59, Aya 7.
MUKHTASARI NA HATIMA.
Hizi ni baadhi ya riwaya tu ambazo zinaonesha kwamba kupunguza rakaa za sala si ruhusa bali ni wajibu. Ziko riwaya nyengine zaidi ambazo pia watetezi wa rai hii wanajenga hoja kwazo kama riwaya ya Ibn Umar “Tumeamrishwa kusali rakaa mbili katika safari,” na riwaya nyengine, lakini hizi chache tulizozitoa zinatosha, bali moja inatosha cha muhimu iwe sahihi. Katika makala yetu ya pili – Inshaa Allah – tutazungumzia hoja za kundi la pili kundi la wanaoona kwamba kupunguza rakaa ni ruhusa tu: si lazima. Halafu tutazungumzia masafa ambayo mtu akiyakata anatakiwa asali safari, na tutaishia kwa kuzungumzia muda ambao mtu anazingatiwa kuwa ni msafiri. Yote hayo yatafanyika Allah akipenda. Na minhaj (methodology) yetu katika mas-ala haya ni uchambuzi wa hadithi tu, kwani ndio msingi. Ama maneno ya wanavyuoni tutayanukuu tukiyahitaji lakini ikiwa yatapinga hadithi basi tutachukua wasia wa Al-imamu Al-shafi na Malik na wengine kwamba “Maneno hayo tuyapige na ukuta.”
Ufupisho wa maudhui ni kuwa:
1) Maudhui yetu ya asili ni kuhusu sala ya safari: je mtu anapokuwa katika safari ni lazima apunguze rakaa au hilo la kupunguza rakaa ni ruhusa tu?
2) Baadhi ya Waislamu wanaona kwamba hio ni ruhusa tu na baadhi wanaona kwamba hio ni lazima.
3) Wanaona kwamba hio ni lazima wanajenga hoja kwa riwaya tafauti ambazo zinasema au zinaonesha kwamba kupunguza rakaa ni wajibu. Miongoni mwa riwaya hizo ni riwaya:
a) Sayyida Aisha inayosema: "ÝÑÖÊ ÇáÕáÇÉ ÑßÚÊíä ÑßÚÊíä ÝÒíÏ Ýí ÕáÇÉ ÇáÍÖÑ æ ÃÞÑÊ ÕáÇÉ ÇáÓÝÑ" “Ilifaradhishwa Sala (mwanzo) rakaa mbili mbili, kisha ikaongezwa sala ya Hadhar (isiokuwa ya safari) na sala ya safari ikaachwa hivyo hivyo (rakaa mbili mbili,” pamoja na matendo ya Mtume (s.a.w.) kwamba yeye hakuwahi hata siku moja kusali kamili katika safari, na hili halina khilafu katika Umma. Hii tumeinukuu nakuitolea maelezo kwa urefu na kuifanyia mukhtasari.
b) Riwaya ya Ibn Abbas. Maana ya riwaya hii ni sawa na riwaya ya Aisha.
c) Riwaya ya Ya’ala bin Umaya kutoka kwa Sayyidna Umar, ambapo Mtume (s.a.w.) katuamrisha tuipokee sadaka ya Allah. Na amri ya Allah na Mtume wake “Zinamaanisha wajibu.”
d) Riwaya ya Umar (r.a.) ambayo anasema ndani yake kwamba katika safari zimefaradhishwa rakaa mbili.
4) Katika mukhtasari juu ya hadithi ya Aisha tulisema maneno ambayo hatuna budi kuyakariri katika mukhtasari huu. Nayo ni kuwa:
a) Wanaoona kwamba kupunguza ni ruhusa tu: si lazima, wamejibu kwa hoja ambazo tumezinukuu, na wapinzani wao wamejibu kwa hoja ambazo tumezinukuu pia.
b) Upinzani walioutoa wale wanaona kuwa hio ni ruhusa, si madhubuti kwani kila hoja yao moja ni kinyume na kanuni za kiusuli na kanuni za elimu ya Hadithi ambazo ndizo tunazojiongozea katika kuifasiri Qur-an na Suna za Mtume (s.a.w.), na aliyesoma fani hizo anaona hivyo kwa uwazi katika majibizano haya au mjadala huu mfupi.
c) Kwa hivyo tunaishia kwa kusema kwamba Hadithi Aisha na hadithi za Masahaba wengine zimethibitisha ulazima wa kupunguza rakaa katika safari, na hakuna hoja madhubuti ya kuzipinga. Kwa hivyo tunasema kwamba Hadithi ya Aisha: “Ilifaradhishwa Sala (mwanzo) rakaa mbili mbili, kisha ikaongezwa sala ya Hadhar (isiokuwa ya safari) na sala ya safari ikaachwa hivyo hivyo (rakaa mbili mbili), pamoja na riwaya za Umar, Ya’ala bin Umaya na Ibn Abbas, ukichanganya na hoja ya kwanza kwamba Mtume (s.a.w.) hajawahi kukamilisha rakaa katika sala ya safari tunapata kwamba kupunguza rakaa ni wajibu kwa mujibu wa suna ya kauli na suna ya vitendo.
Inshaa Allah, itafata sehemu ya pili “Hoja za waliosema kwamba kupunguza ni rusa tu: si lazima.”
Ahsante:
Ibn Moh’d Al-mazrui.